Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli leo aliungana na watanzania katika sherehe ya kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru katika kiwanja cha CCM Kirumba Mkoani Mwanza
Katika sherehe hiyo Mh.Rais alisisitiza suala zima la Amani, Umoja na Mshikamano ambao vilipiganiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa naviongozi wenzake katika harakati za kulikomboa taifa hili.
Maadhimisho hayo ni ya tano tangu serikali ya awamu ya tano kuongia madarakani.
Aidha, Mh. Rais alitoa msamaha kwa wafungwa idadi 5533 kutoka magereza mbalimbali yaliyopo nchini.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.