Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa tano wa makamanda tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Brigedi ya Chui Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa kutoa neno la utangulizi katika mkutano huo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo alisema, Hali ya Ulinzi wa mipaka ya nchi ni shwari, wapiganaji wanaendelea kuhakikisha mipaka inakuwa salama na kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.
Pia, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Stargomena Lawrence Tax, alimshukuru Rais kwa kukubali kufungua Mkutano na hii imewapa morali Makamanda. Alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu kwa kuliwezesha Jeshi kwa kulipatia zana, mafunzo na kuzingatia maslahi ya wanajeshi, lengo ni kuendelea kuimarisha Ulinzi na usalama wa Mipaka.
Akizungumza na Makamanda wa JWTZ, Mhe. Rais amelipongeza Jeshi kwa kuendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi na kusema kuwa, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania litaendelea kulinda uhuru na mipaka ya nchi kwa kuzingatia umahiri na nidhamu wakati wote wa kutekeleza wajibu wake.
Aliongeza kuwa, amani na usalama ni msingi wa maendeleo katika taifa hivyo Jeshi liendelee kusimamia Amani ili kuwafanya wawekezaji kuwa na uhakika wa usalama kwa kuwekeza mitaji yao na serikali kupanga shughuli za maendeleo.
Mkutano huo unaendeshwa na Mkuu wa Majeshi kujadili na Makamanda kuhusu ulinzi na masuala ya Taifa.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.