• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Brigedia Jenerali Mabele Mkuu wa JKT

Brigedia Jenerali Mabele Mkuu wa JKT Posted On: Wednesday, 19th May 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Mei 2021 amemteua Brigedia Jenerali Rajabu Nduku Mabele kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa. Hatua hiyo inafuatia kuteuliwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Charles Mbugekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera hivi karibuni.

Brigedia Jenerali Mabele alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 25 Novemba 1993 na kutunukiwa Kamisheni kuwa Afisa tarehe 25 Machi 1995. Pamoja na taaluma nyingine za Kijeshi, Jenerali Mabele ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (Master of Business Administration), alijikita katika Usimamizi wa Mashirika (Corporate Management).

Katika utumishi wake Brigedia Jenerali Mabele amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Afisa Usalama na Utambuzi katika Vikosi kadhaa; Afisa Mnadhimu Malipo na Afisa Malipo wa Kikosi Makao Makuu ya Jeshi; Mkurugenzi wa Fedha za Umma na Uhasibu (Director for Public Finance and Accounting) na baadae alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT), nafasi aliyohudumu hadi kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Sambamba na uteuzi huo, Mhe. Rais amemteua pia Kanali Absolomon Lyanga Shausi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA-JKT. Kabla ya uteuzi huo Kanali Shausi alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo.

Kwa niaba ya Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anawapongeza Brigedia Jenerali Mabele na Kanali Shausi kwa kuaminiwa katika nyaadhifa hizo na kuwatakia heri na fanaka katika utendaji wao.


Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 2
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 3
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea mwezi 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.