Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amekipongeza Chuo cha Taifa cha Ulinzi kwa kuanzisha mitaala mipya ya kuwasaidia viongozi wa Serikali ngazi ya kati.
Ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya Miaka Kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012.
Amesema masomo hayo yataongeza ufanisi mkubwa kwa viongozi hao kwani wataweza kuendana na mawazo ya Serikali Kuu hasa katika suala zima la Ulinzi wa Taifa katika kuiletea nchi maendeleo chanya.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa elimu ya ulinzi na stratejia ndio njia pekee ya kuishindana na changamoto za kidiplomasia na uchumi hivyo ni lazima ipewe kipaumbele.
Kabla ya hotuba yake, Mhe. Rais na Amir Jeshi Mkuu alitunukiwa Tuzo ya Heshima kwa kutambua mchango wake katika kuboresha na kuendeleza Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Maadhimisho hayo ya Miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa Chuo Cha Taifa cha Ulinzi yamehudhuriwa na Mabalozi, Waambata Jeshi kutoka nchi rafiki, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania wastaafu.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.