Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Salvatory Venance Mabeyo nishani maalum ya Mlima Kilimanjaro (University of Iringa Mount Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika "campus" ya Chuo Mjini Iringa tarehe 28 Nov 20.
Mwingine aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho mwaka 2019.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.