Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo amewataka wakuu wa vikosi vya JWTZ na JKT kuwa wabunifu katika kubuni miradi mbalimbali ya kibiashara ili Kujenga uwezo wa kifedha wa kuhudumia shughuli mbalimbali za Kijeshi ikiwemo Mafunzo ya Vijana.
Jenerali Mabeyo ameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba wakati akizindua kituo cha burudani kilichojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa kilichopo katika eneo la Medel East katikati yaJijini la Dodoma.
Amesema uzinduzi wa kituo hicho uwe chachu kwa wakuu wa vikosi na wote wenye nafasiya kufanya maamuzi kubuni mikakati yakufikiriamiradi ya maendeleo.
Aidha amelipongeza JKT kwa ubunifu wa Kituo hicho na kutaka majengo ambayo bado hayajamalizika kujengwa yaharakishwe ili Ukumbi huo uwe wa mfano hapa jijini Dodoma.
Naye Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele amesema Kituo hicho kitawezesha Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma na Wananchi wa Dodoma kutumia ukumbi huo katika shughuli zao mbalimbali kama mikutano ambapo shughuli hizozitawezesha kituo hicho kujipatia fedha zitakazosaidia kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia Jeshi hasa katika malezi ya vijana.
Ameongeza kuwa Fedha za ujenzi wa kituo hicho zimetokana na faida ya miradi mbalimbali iliyo chini ya JKT.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.