Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda Leo amefungua rasmi Kikao cha 33 cha Mwaka cha Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Jumuhiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Arusha Tanzania.
Jumla ya Wakuu wa Majeshi idadi 12 Miongoni mwa 16 kutoka Nchi Wanachama wa SADC Wameshiriki Kikao hicho ambacho Mwenyekiti wake ni Jenerali Jacob John Mkunda Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania.
Ufunguzi huo rasmi uliofanyika leo tarehe 30 Mei 2025 ulitanguliwa na hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Makonda
aliyezungumza na hadhara hiyo akiwakaribisha nchini Tanzania na kufikisha Salamu za Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Daktari Samia Suluhu Hassan.
Kufanyika kwa Mkutano huo hapa nchini ni kufuatia kuchaguliwa kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi August 2024 kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC.
Kutokana na Uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi Tanzania alichukua nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Wakuu wa Majeshi na Mwenyeji wa Kikao hicho.
Pamoja na ajenda zingine, Kikao hicho kimepokea na Kujadiri masuala yote yahusuyo Ulinzi na Usalama Katika Kanda Kwa Kipindi Cha Mwaka mmoja kuanzia Mei 2024 hadi Mei 2025.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.