Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea Meli Tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika.
Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ .
Meli tiba ya Jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye Bandari ya Dar es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa Wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZna ushirikiano wa Miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu waChina.
Matibabu hayo yalianza kutolewa Tarehe 18 Julai 2024 hadi Tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini Tarehe 23 Julai Mwaka huu.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.