Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda leo ameanza ziara ya kutembelea na kufanya ukaguzi wa Vikosi, Vyuo na Shule za Kijeshi Mkoani Arusha ili kujionea utayari wa Kivita na Mafunzo.
Katika ziara yake Jenerali Mkunda ameambatana na Majenerali wa Makao Makuu ya Jeshi ili kusikiliza kwa pamoja changamoto zilizopo na kuzitatua papo kwa papo.
Jenerali Mkunda ameridhishwa na utayari wa Vikosi vyote kimafunzo na kivita ambapo ameviagiza Vikosi vyote nchini kufanya mafunzo kwa nguvu zote ili kuwa tayari kulinda nchi na Wananchi wote.
Katika ziara yake amefungua Zahanati katika Kambi ya JKT Makuyuni yenye uwezo wa kulaza wagonjwa wakiwemo Wanajeshi, Vijana wa JKT na wananchi wengine. Aidha, amezindua Mabwalo mapya ya Maafisa na Askari katika Vikosi hivyo na amewataka waishi na kudumisha ushirikiano na vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.