Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) katika juhudi zake za kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini hususan Jiji la Dar es salaam nakutaka kuendelezwa juhudi hizo ili kutokomeza maradhi ya maambukizi nchini.
Amesema kambi ya Lugalo imekuwa mfano mzuri kwa Raia na wageni kwa jinsi walivyofanikiwa kutunza mazingira na maua na kutaka taasisi zingine kuiga mfano huo
Mapema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akimkaribisha Mh. Makonda amewataka Wananchi wanaotumia uwanja wa Mwenge kufanyia biashara ya vinyago kuboresha vibanda vyao ili vionekane na hadhi inayoendana na biashara yao kwani wateja wao wengi ni kutoka nje ya nchi na pia kukumbushia kutunza mazingira ya eneo hilo.
Sherehe hizo zilipambwa na michezo mbalimbali kama mpira wa miguu, maonesho ya mbwa, mazingaombwe na burudani kutoka vikundi mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 tokea kuundwa kwa JWTZ.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.