Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo tarehe 21 Agosti 2020 limewaaga Majenerali waliostaafu rasmi utumishi kwa kutimiza umri wa lazima.
Kama ilivyo mila na desturi za Jeshi, Majenerali hao waliagwakwa gwaride rasmi katika viwanja vilivyopo katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo Mgulani jijijni Dar es Salaam.
Sherehe hizo za kuwaaga Majenerali hao zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Salvatory Mabeyo na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Yakubu Mohamed. Aidha viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa Majeshi wa tano Jenerali Robert Mboma (Mstaafu), Mkuu wa Majeshi wa Sita Jenerali George Waitara (Mstaafu), wanadhimu wakuu wastaafu akiwemo Luteni Jenerali Martin Mwakalindile , Luteni Jenerali Samwel Ndomba, Luteni Jenerali James Mwakibolwa na viongozi wengine wa kijeshi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Luteni Jenerali Paul Massao aliwataka Watanzania kuendelea kuitunza na kuienzi tunu tuliyopewa ya amani na utulivu nchini kwani ndio msingi pekee uliopelekea Tanzania kufika malengo ya kuwa na uchumi wa kati kwa kuwavutia wawekezaji. Aidha, aliwataka Maafisa na Askari wanaoendelea kulitumikia jeshi waendeleze nidhamu, uadilifu, utii na uhodari kwani ndizo nguzo pekee za jeshi lenye kuhitaji mafanikio na kuijenga taswira chanya ndani na nje ya nchi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.