Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kushirikiana na Jeshi la Marekani wamefungua Mafunzo Maalum ya kukabiliana na Vitendo vya Uhalifu ikiwemo Ugaidi na Uharamia. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 28, 2021 katika kituo cha Ulinzi wa Amani kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi huo alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Afrika wa Jeshi la Marekani, Jenerali Stephen Townsend. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Jenerali Townsend amesema Tanzania na Marekani zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya kijeshi.
Kwa Upande wake Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amesema Jeshi la Marekani limekuwa likishirikiana vyema na JWTZ katika nyanja mbalimbali.
Kufanyika kwa mafunzo hayo kutasaidia kuwaongezea uwezo Maafisa na Askari wa JWTZ katika kukabiliana na vitendo vya Uhalifu, hivyo ulinzi wa nchi kuimarika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.