Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Mwinyi (MB) leo tarehe 23 Oktoba 2019 amefungua rasmi kitengo kipya cha matibabu cha kusafisha figo (Dialysis) katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Jeshi katika kuboresha utoaji wa huduma ya afya nchini.
Aidha, Waziri Mwinyi alimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (mstaafu) kwa kuanzisha wazo hilo na kuungwa mkono na wasaidizi wake akiwemo Mkuu wa Majeshi wa sasa Jenerali Venance Mabeyo kwa kuliendeleza wazo hilo mpaka kufikia hatua hii ya kuanza kutoa huduma ya matibabu ya kusafisa figo.
“Kufunguliwa kwa jengo na utoaji wa huduma hii katika Hospitali ya Jeshi, itapunguza gharama kwa Jeshi kwani Maafisa, Askari, familia zao na watu wengine wataipata huduma hii hapahapa nchini na kwa bei nafuu zaidi na hivyo kuweza kuokoa maisha ya watanzania walio wengi ambao walikuwa wanashindwa kuwapeleka ndugu zao nje ya nchi”.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo aliwataka wataalamu wa kitengo hicho kuwa makini katika utendaji wa kazi kwani suala la tiba ya figo linahitaji umakini mkubwa. Kwamujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Jeshi Lugalo Brigedia Jenerali Gabriel Mhidzealisema kitengo hicho kipya cha usafishaji wa figo kinauwezo wa kuhudumiawagonjwa wa figowasiopungua 40 kwa siku, ambapo katika mashine kumi zilizofungwa katika kitengo hicho kila mashine inauwezo wa kuhudumia wagonjwa wasiopungua watano (5).
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.