Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Methew Mkingule amefanya ziara ya kikazi ya kukagua Mipaka ya Kusini na kutembelea Kikundi cha Askari wa Tanzania walioko katika Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika nchini Msumbiji (SADC Mission in Mozambique).
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujionea utendaji kazi wa Vikundi vya JWTZ vinavyotekeleza majukumu yake na pia kujitambulisha katika nafasi yake ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ toka ateuliwe na Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi Agosti Mwaka jana.
Aidha, Luteni Jenerali Mkingule aliwapongeza Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Songea na Mtwara kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa katika Ulinzi wa nchi na kusimamia miradi yao katika Vikosi.
Alisisitiza Wanajeshi wote kuendelea kukiishi kiapo kwakua ndio msingi mkubwa katika kulilinda Taifa.
Luteni Jenerali Mkingule aliongeza kwamba kila mmoja aliapa kulilinda na kulitetea Taifa na hakuna Taifa lingine zaidi ya Tanzania na amewaasa wanajeshi juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.