• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa Posted On: Saturday, 7th June 2025

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania limeandaa Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa lililofanyika katika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha tarehe 6 Juni 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman amekipongeza Chuo hicho kwa kutengeneza jukwaa muhimu kwa wanataaluma ili kujadili maswala mtambuka hasa wakati huu ambapo kuna matishio mbalimbali yanayoikabili Dunia.

Aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kujadiliana kwa kina mada zinazowasilishwa ili kuja na suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa kwa sasa na kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Meja Jenerali Justice Stephen Mnkande amesema kuwa Kongamano hilo ni la kwanza kuandaliwa na Chuo hicho likilenga mada tatu ambazo ni matumizi ya Akili Mnemba katika Ulinzi wa Taifa,Usalama wa Chakula kama Msingi wa Uimara wa Taifa na Usalama wa Nishati kwaajili ya Maendeleo Endelevu ya Taifa kwakuwa maeneo haya matatu yasipoangaliwa kwa kina yanaweza kuhatarisha Usalama wa Taifa.

Amesisitiza kuwa Kongamano hilo litakuwa Endelevu ili kutoa fursa kujadiliana maswala mbalimbali yahusuyo Ulinzi na Usalama wa Taifa letu.Aidha amesema kuwa makongamano yatakayoandaliwa baada ya hili yatakuwa ya kimataifa yakihusisha viongozi na wanataaluma kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana uzoefu katika kukabiliana na matishio hayo

Kongamano la kwanza la Usalama wa Kitaifa limewakutanisha Makamanda kutoka JWTZ,viongozi waandanizi wa Serikali,wataalam bobezi katika nyanja mbalimbali kutoka ndani na nje ya chi na Wanafunzi wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu kundi la 39 la mwaka 2024 hadi 2025.

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 1
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 2
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea wiki 4
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.