Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amehutubia mamia ya watanzania leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Sherehe hizo zilipambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania, vikundi vya ngoma , gwaride la watoto wa shule za msingi na wasanii mbalimbali kutoka hapa nchini. Aidha, makomando wa JWTZ wakati wa maadhimisho hayo walionesha umahiri wa hali ya juu wa namna viongozi (VIP) wanavyookolewa.
Vile vile Rais na Amiri Jeshi Mkuu ametoa msamaha kwa wafungwa 8157ambapo wafungwa 1828 wameruhusiwa kuanzia leo na waliobaki wamepunguziwa muda wa vifungu vyao.Hivyo watatoka kulingana na vifungo hivyo
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.