Mkuuwa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu kutoka nchini India Jenerali Bipin Rawat ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi mapema leo amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopo Upanga Jijini Dar es Salaam.
Akiwa Makao Makuu ya Jeshi, Jenerali Rawat alipata fursa ya kukutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Hussein Mwinyi (Mb) ofisini kwake.
Jenerali Rawat anatarajiwa kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.