Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo ametembelea na kuzungumza na Maafisa na Askari wa Kanda ya Mwanza tarehe 8 Februari 2021.
Akizungumza na Maafisa na Askari wa Kanda hiyo, Mkuu wa Majeshi amesisitiza umuhimu wa kudumisha nidhamu katika utendaji kazi na pia kuzingatia kiapo cha utii kwa mwanajeshi kwani ndicho kinachotuongoza kwenye majukumu yetu ya kila siku.
Kabla ya kikao hicho Jenerali Mabeyo alitembelea vikosi mbalimbali vilivyopo katika kanda hiyo na kujionea utendaji kazi wa vikosi hivyo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.