Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo Oct 10 alifanya ziara kutembelea maeneo ya Selous katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji mkoani Pwani ambapo mradi mkubwa wa Stiegler’s Gorge unatarajiwa kujengwa ili kuzalisha umeme wa megawati 2,000 zitazosaidia kutatua tatizo la umeme hapa nchini.
Akiwa katika mradi huo Jenerali Mabeyo alisema kuwa amefarijika na hatua ya Serikali kulishirikisha JWTZ katika miradi mbalimbali ili nalo liweze kujiandaa vyema katika jukumu zima la ulinzi wa rasilimali za taifa.Aidha, kushirikishwa huko ni chachu ya maendeleo katika ujenzi wa viwanda vya uzalishaji na kutoa fursa kwa Watanzania kupata ajira.
Vile vile Jenerali Mabeyo alipata fursa ya kutembelea eneo la Stesheni ya Fuga ya Tazara ambapo itakuwa ni kituo kikuu cha kupokelea na kuhifadhi vifaa vya ujenzi wa mradi huo.Pia aliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua ya kutengeneza miundombinu ili kuhakikishaeneo la mradi linafikika kwa urahisi.Mradi huo unatarajiwa kuchukua takribani miezi 36 hadi kukamilika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.