• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Mkuu wa Majeshi aongea na Maafisa na Askari

Mkuu wa Majeshi aongea na Maafisa na Askari Posted On: Friday, 18th December 2020

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo leo tarehe 17 Disemba, 2020 amezungumza na Maafisa na Askari wa Kikosi cha Ndege za Usafirishaji kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kikosini hapo Jenerali Mabeyo aliwapongeza Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2020, kwani uchaguzi umeisha salama na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii huku wakikumbuka viapo vyao kila wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Aidha, amesema kuwa mafanikio tulioyapata ni matokeo ya kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano, utii, uadilifu na kujituma. Jenerali Mabeyo amesisitiza kuwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawahakikishia wananchi kuwa Taifa lipo salama na waendelee kufanya shughuli zao ili kujiletea maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa Wanajeshi wanapaswa kutojihusisha na masuala ya kisiasa na udini kwani vinaweza kuligawa Jeshi na kupelekea uwepo wa makundi na kuondoa umoja uliopo.

Kuhusu ugonjwa wa Corona, Mkuu wa Majeshi amewataka Maafisa, Askari na Familia zao kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo. " Tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezimungu kwani yapo Mataifa mengi yameathirika na ugonjwa huu, lakini sisi ametuepusha na janga hili" alisema Mkuu wa Majeshi.

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 2
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 3
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea mwezi 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.