Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Burundi Luteni Jenerali Niyongabo Prime leo Novemba 08, 2017 amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam, ziara hiyo imelenga kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya Majeshi ya nchi hizi mbili.
Mkuu wa Majeshi huyo amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo katika Viwanja vya Wizara ya Ulinzi na JKT na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na JWTZ kwa ajili yake. Aidha baadaye alifanya mazungumzo ofisini kwa mwenyeji wake.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.