Mkuu wa Majeshi ya visiwa vya Comoro Kanali Youssouf Idjihadi hivi karibuni amefanya ziara ya kikazi hapa nchini ambapo wakati wa ziara hiyo alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo kiwanda cha ushonaji wa mavazi ya kijeshi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam na shirika la nyumbu lililopo Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu wa Majeshi huyo alipokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo na kisha kufanya mazungumzo ofisini kwake ambapo lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kubadilishana uzoefu na kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili. Aidha Kanali Idjihadi alipata nafasi ya kumtembelea Waziri wa Ulinzi na JKT Mh. Dkt. Hussein Mwinyi ofisini kwake.
Vile vile akiwa katika kiwanda cha ushonaji cha JKT Mkuu wa Majeshi ya Visiwa vya Comoro aliweza kujionea jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi zake
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.