• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Mnadhimu Mkuu atembelea Vikosi na Shule

Mnadhimu Mkuu atembelea Vikosi na Shule Posted On: Thursday, 23rd September 2021

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Methew Mkingule amefanya ziara katika vikosi vilivyopo mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha kwa Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma waliopo katika vikosi hivyo baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo. Sambamba na kujitambulisha Mnadhimu Mkuu alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikosi hivyo.

Aidha, aliwataka Maafisa na Askari kutojihusisha na siasa. Pia kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwani vitendo hivyo vinaweza kuharibu taswira ya Jeshi. Vilevile alisisitiza kuwa Jeshi halimzuii Afisa au Askari kutumia mitandao ya kijamii kama atakuwa anaitumia kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yenye faida kwake binafsi na Jeshi kwa ujumla.

"Atakayebainika kutumia vibaya mitandao ya kijamii, kujihusisha na mambo ya siasa au vitendo vya aina yoyote ile vinavyokwenda tofauti na mila, desturi, utaratibu, maelekezo na sheria za nchi na zile za kijeshi, Jeshi halitasita kumchukulia hatua za kinidhamu" alisema Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Mkingule.

Akizungumzia suala la nidhamu, Mnadhimu Mkuu aliwataka viongozi katika ngazi mbalimbali wasimamie nidhamu vikosini kwani nidhamu ndio uti wa mgongo wa Jeshi letu. " Leo hii Jeshi letu linapata sifa nzuri ndani na nje ya nchi linapotekeleza majukumu mbalimbali, hii ni kwa sababu ya nidhamu inayooneshwa na Wanajeshi wetu wanapokuwa kwenye majukumu mbalimbali. Aliwataka Wakuu wa Vikosi na Shule kuhakikisha wanasimamia nidhamu ya Maafisa na Askari walio chini yao ili kujenga Jeshi mahiri, hodari nalenye weledi" alisema Mnadhimu Mkuu.

Vilevile Luteni Jenerali Mkingule aliwapongeza Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma kwa mafanikio mazuri yanayotokana na miradi mbalimbali inayoendeshwa sehemu mbalimbali. Pia aliwataka kuendelea kudumisha ushirikiano mzuri uliopo baina yao na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na raia wanaoishi maeneo ya jirani na Vikosi vyao.

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 2
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 3
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea mwezi 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.