Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othuman amefungua rasmi kikao cha 20 cha Huduma za Afya kwa Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Arusha.
Luteni Jenerali Othman amewata wanadhimu washiriki wa kikao kutathminihuduma za afya kwa Majeshi yao ili kwenda na hali ya kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza duniani.
Alieleza kuwa kwa sasa hali ya Maambukizi ya COVID-19 nchini ni kidogo ukilinganisha na hapo awali ambapo kwa sasa, wananchi wa Tanzania wanaendelea na shughuli za uzalishaji sambamba na kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo.
Aidha, amewataka washiriki wa kikao hiki kujiona wapo nyumbani kwani Tanzania kuna ukarimu kwa wageni, na wajiandae kwenda kutembelea mbuga za wanyama kujionea vivutio vya utalii na utamaduni wa kabila la kimasai baada ya kumaliza kikao.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.