• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi...
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi...
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma...
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni...
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu...
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI Posted On: Wednesday, 31st July 2024

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita. Aidha, uandikishaji utahusisha vijana waliopo katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa 'Operesheni Jenerali Venance Mabeyo' na waliomaliza mkataba ambao wamefanya mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na kwa Mkataba wa kujitolea.

Vijana wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Awe raia wa Tanzania.

Awe na umri usiozidi miaka 25.

Awe na afya nzuri na akili timamu.

Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa.

Awe na cheti halisi cha kuzaliwa.

Awe na vyeti vya shule.

Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo.

Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) au mafunzo ya Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NI IFUATAVYO:-

Kwa vijana waliopo katika makambi ya JKT 'Operesheni Jenerali Venance Mabeyo' taratibu zao zinaratibiwa na Makao Makuu ya Jeshi.

Kwa vijana waliopo nje ya Makambi ya JKT, maombi yao yaandikwe kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi, Dodoma kuanzia tarehe 01 Agosti, 2024 hadi tarehe 14 Agosti, 2024 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-

Nakala ya kitambusho cha Taifa au namba ya NIDA.

Nakala ya cheti cha kuzaliwa.

Nakala za vyeti vya Shule.

Nakala ya cheti cha JKT.

Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.

MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO:

Mkuu wa Utumishi Jeshini,

Makao Makuu ya Jeshi,

Sanduku la Posta 194,

DODOMA, Tanzania

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 2
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 3
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea mwezi 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.