• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Pumzika kwa Amani Mwana wa Afrika

Pumzika kwa Amani Mwana wa Afrika Posted On: Monday, 22nd March 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 22 Machi 2021 ameongoza maelfu ya watanzania jijini Dodoma na mikoa jirani katika siku ya tatu ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini humo.

Shughuli hizo zimefanyika kitaifa jijini humo ambapo zilipambwa na gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa, Maafisa Wanafunzi na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Aidha sherehe hizo zilihudhuriwa na marais kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kenya, Msumbiji, Visiwa vya Comoro, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika Kusini na wawakilishi kutoka katika nchi za Burundi, Rwanda na Namibia.

Viongozi hao walipata fursa ya kutoa salamu za rambirambi na kuwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu, na kudumisha amani iliyopo nchini. Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Uhuru Kenyatta aliwataka Watanzania kumpa ushirikiano Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha uongozi wake ili kuweza kuyakamilisha yale yote yaliyoachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza na Watanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwatoa hofu Watanzania kwa kuwahakikishia kuwa yeye atayaendeleza yale yote ambayo ameyaacha mtangulizi wake kwa maslahi ya nchi.

Habari Mpya

  • Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    Luteni Jenerali Othman ashiriki Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa

    tokea wiki 2
  • Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    Jenerali Mkunda afungua Kikao cha Wakuu wa Majeshi SADC

    tokea wiki 3
  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea mwezi 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea mwezi 1
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.