Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewatunuku kamisheni Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika sherehe iliyofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha tarehe 18 Novemba 2023.
Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Jackson Jairos Mwaseba amesema Maafisa hao wapya waliotunukiwa kamisheni wamehudhuria Mafunzo hapa nchini na kwenye vyuo vya Kijeshi katika mataifa rafiki. Aidha alisema kuwa katika kundi hilo Maafisa wanawake 93 wametunukiwa kamisheni.
Mbali na kutunuku kamisheni Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu aliwatunuku Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi Maafisa 62 ambapo kwa mara ya kwanza Shahada hiyo imetolewa kwa kusimamiwa na Chuo hicho bila ushirikiano na Chuo cha Uhasibu Arusha.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda aliwataka Maafisa wapya kuviishi viapo walivyoapa ili waweze kutoa mchango wenye matokeo chanya katika kulitumikia Taifa wakiwa Maafisa ndani na nje ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.