• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • Kiswahili
  • English

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

  • Kuhusu Sisi...
    • Historia
    • Dira,Dhima na Majukumu
  • Kujiunga na JWTZ
  • Kamandi...
    • Kamandi ya Jeshi la Wanamaji
    • Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu
    • Kamandi ya Jeshi la Anga
    • Jeshi la Kujenga Taifa
    • Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi
    • Kamandi ya Jeshi la Akiba
  • Huduma...
    • Afya
    • Elimu
    • Michezo
    • Viwanda
  • Oparesheni...
    • Endelevu
    • Iliyokamilika
  • Kumbukumbu...
    • Video
    • Picha
    • Hotuba

Rais Samia Suluhu Hassan azindua hospitali ya JWTZ

Rais Samia Suluhu Hassan azindua hospitali ya JWTZ Posted On: Wednesday, 28th July 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la nchi hiyo (GAFTAG) iliyojengwa maalum kwa ajili ya magonjwa ya milipuko na yasiyoambukiza Lugalo jijini Dar es salaam.

Aidha, Rais Samia amepongeza uongozi wa JWTZ chini ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kwa kujituma na kulinda mipaka ya nchi kikamilifu sambamba na kuitangaza nchi kimataifa kwa kushiriki ulinzi wa amani katika mataifa mbalimbali. Vilevile, amesema kituo hicho cha kipekee kimekuja wakati muafaka na kulitaka JWTZ likitunze kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mabeyo amesema mradi huu unaenda sambamba na miradi mingine ya JWTZ iliyotekelezwa kwa msaada wa Jeshi na Serikali ya Ujerumani.

Jenerali Mabeyo ameitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na Karakana ya magari iliyopo Lugalo jijini Dar es Salaam, Hospitali zaJeshi za Kanda na Kituo cha Ulinzi wa Amani.

Naye Balozi wa Ujerumani nchini Bi Regina Hess amesema lengo la mradi huu ni kuliwezesha JWTZ kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza. Aidha amesema, Serikali ya Ujerumani inategemea kukamilisha mradi mwingine mkubwa wa hospitali jijini Dodoma.

Uzinduzi wa hospitali hiyo yenye majengo na vifaa vyenye uboraimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe pamoja na Wakuu wa Matawi wa JWTZ.

Habari Mpya

  • Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha  Ushirikiano

    Afrika Mashariki Yaendelea Kuimarisha Ushirikiano

    tokea wiki 1
  • ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    ​Jenerali Mkunda aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kokoto Arusha

    tokea wiki 3
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    TANGAZO LA NAFASI ZA KUANDIKISHWA JESHINI

    tokea wiki 3
  • ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    ​Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo Askari Wapya

    tokea wiki 4
  • Zaidi

Nifanyeje

  • Utaratibu wa kujiunga na JWTZ tokea miaka 8
  • Majukumu ya Msingi ya JWTZ tokea miaka 8
  • Wakuu wa Majeshi waliopita JWTZ tokea miaka 8
  • Wanadhimu Wakuu waliopita JWTZ tokea miaka 2
  • Zaidi

Wasiliana Nasi

Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz

Kurasa za Karibu

  • Marais walioongoza Tanzania
  • Tangazo kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria 2016
  • Taarifa kuhusu vijana kujiunga na JKT

Tovuti Mashuhuri

  • Shirika la Uzalishaji Mali - SUMAJKT
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Kujenga Taifa
  • Wizara ya Ulinzi na Kujenga Taifa
  • Chuo cha Ulinzi wa Taifa - Tanzania

Jarida la Ulinzi

Zaidi

Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.