Kwa niaba ya Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anatoa pole kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu kwa msiba mkubwa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano na Amiri Jeshi Mkuu, Hayati Dkt, John Pombe Joseph Magufuli.
Pamoja na mafanikio mengi mengine, Hayati Dkt. Magufuli atakumbukwa kwa uongozi makini; kupambana na rushwa; kujenga nidhamu ya kuchapa kazi; nidhamu ya ukusanyaji kodi na matumizi bora ya fedha; kuyahamishia Makao Makuu Dodoma; kujenga miundombinu ya afya, elimu, barabara, madaraja, umeme; kutoa elimu bila kulipia hadi kidato cha nne; ujenzi wa Meli, sambamba na kuanzisha miradi ya kimkakati ya SGR,Bwawa la Umeme la Nyerere, kufufua ATCL na kuhamasisha uchumi wa viwanda hadi kuiingiza Tanzania kwenye Uchumi wa Kati.
Mungu ailaze Roho ya Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mahali pema peponi, Amina.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.