Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Tanzania ni miongoni mwa Vyuo bora Afrika na Duniani ambavyo vinatoa mafunzo ya Usalama na Stratejia ya Kitaifa na Kimataifa. Hivi karibuni Chuo kimefanya Mahafali ya Saba tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012.
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Jumla ya wahitimu 39 wakiwemo Maafisa wa ngazi za juu kutoka katika nchi kumi na moja ikiwemo Tanzania, Botswana, Burundi, China, Kenya, Misri, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Zambia pamoja na Zimbabwe. Kutoka nchini washiriki wa kozi hiyo walitoka kwenyeVyombo vya Ulinzi na Usalama, Serikalini na Taasisi nyingine za Serikali na wahitimu hao waliweza kutunukiwa Stashahada na Shahada ya Uzamili.
Aidha, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia aliwataka wahitimu watakaporudi katika nchi zao kuweza kuzishauri Serikali na Majeshi ya nchi wanazotoka kusimamia suala la amani ili kuondoa migogoro mbalimbali iliyopo katika nchi zao, kwani wamepewa nyenzo zote za kwenda kufanya kazi na kusaidia Serikali zao kutunga sera zitakazosaidia kutunza amani, utulivu na usalama katika nchi zetu hasa Afrika.
Afrika kuna changamoto nyingi za usalama kwa hiyo wanategemewa wao na wenzao ambao wamepita chuo kama hiki katika kutoa ushauri nchini mwao juu ya nini kifanyike ili Bara la Afrika libaki kuwa salama.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.