Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa siku saba kwa wananchi wanaomiliki sare za Majeshi au zinazofanana nazo kinyume na sheria kuzisalimisha sare hizo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi na Msemaji wa JWTZ Luteni Kanali Gaudentius Ilonda jijini Dodoma.
Luteni Kanali Ilonda amewataka wananchi kuzirudisha sare hizo kwa hiari yao ili kuepusha tafrani inayoweza kujitokeza baada ya kupita muda uliowekwa.
Katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Pamoja na kifungu cha 178 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 (Penal Code) na kifungu cha 6 cha sheria ya Usalama wa Taifa
Vifungu vyote hivyo vinakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ ama zinazoelekea kufanana nazo bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.