Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan amewaongoza watanzania kwa kusherehekea miaka 60 ya Uhuru katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mara baada ya kuingia uwanjani Rais na Amiri Jeshi Mkuu alipigiwa mizinga 21 ya utii na kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Kujenga Taifa, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Uhamiaji.
Sherehe hizo zilizofana zilipambwa na maonesho mbalimbali ya zana vita za JWTZ, pamoja na maonesho ya uokoaji kutoka vikundi maalum vya JWTZ kwa kutumia helikopta.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Marais, Wakuu wa Nchi na wawakilishi kutoka nchi rafiki za Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji, Visiwa vya Comoro, Oman, Uswatini, Burundi, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.