Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewaongoza Watanzania katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa awamu ya tatu Hayati Dkt William Benjamin Mkapa yaliyofanyika kijijini kwao Lupaso katika Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara leo tarehe 29 Julai 2020
Shughuli hizo za mazishi zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi na Raismstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Mhe. Ali Mohamed Shein
Aidha, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuiendeleza misingi aliyoiweka Hayati Mzee Mkapa Rais wa awamu ya tatu kwani yeye ndiye aliyeweka misingi Sera ya kimkakati ya kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa kati ifikapo 2025 na kukuza uchumi wa viwanda.
"Rais Mkapa ndiye aliyeiandaa dira ya kufikia Uchumi wa kati na wa viwanda japo wakati wa utekelezaji wake watu wengi walikuwa wanapiga kelele lakini aliniambia kamwe hawataelewa faida ya hiki ninachokifanya kwa sasa. Nitakuachia mpango huu na uuendeleze kwa wakati wako kwa kuwa mpango huu ni wa muda mrefu mpaka 2025". alisema Dkt Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa Rais aliyepo madarakani Dkt. John Magufuli anajukumu la kuhakikisha analifikia lengo hilo.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.