Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Innocent Bashungwa amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kuonesha utayari wa hali ya juu wa kuilinda mipaka ya nchi ya Jamhri ya Muungano wa Tanzania.
Ameyasema hayo alipotembelea zoezi la Dragon Fly lililofanywa na Kamandi ya Jeshi la Anga Mkoani Lindi.
Amesema kuwa duniani kote Jeshi ni taasisi inayohusika kwenye kuleta maendeleo na teknolojia hivyo ni wakati muafaka sasa wa kufanya jitihada za makusudi ili kuendana na kasi hiyo.
Amesisitiza na kuweka mkazo kwenye mafunzo mbalimbali ya Maafisa na Askari kusimamiwa kikamilifu ili kuwa na Wanajeshi wenye ufanisi na weledi wakati wa amani na vita.
Zoezi la Dragon Fly ni muendelezo wa mazoezi mbalimbali ya kivita yanayofanyika hapa nchi.Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.