Waziri wa Ulinzi na JKT Mheshimiwa Dkt Stergomena Tax amezindua bomu baridi lenye uwezo mkubwa wa kutawanya makundi ya Tembo yanayovamia makazi ya watu wanaoishi karibu na hifadhi za Taifa na mapori ya akiba.
Mheshimiwa Dkt Tax amelishukuru Shirika la Mzinga kwa kutengeneza bomu hilo huku akilitaka Shirika hilo kuendeleza ubunifu ili kuweza kulisaidia Taifa katika kukuza teknolojia. Amesema kuwa bomu hilo litasaidia kupunguza madhara ya uvamizi wa tembo kwani halmashauri 81 zimekuwa zikisumbuliwa na Wanyama hao. Aidha Dkt Taxi amezitaka taasisi zitakazotumia mabomu hayo kuyatumiakwa kuzingatia miongozo ili yasije yakaleta athari kwa watumiaji.
Akitoa taarifa kwa Mheshimiwa Waziri, Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Seif Hamis amesema kuwa bomu lililofanyiwa utafiti na kutengenezwa na Shirika hilo liko katika aina mbili ambapo wametengeneza bomu linaloweza kulipuka likiwa angani na lipo linaloweza kulipuka baada ya kutua ardhini. BrigediaHamis ameongeza kuwa Shirika la Mzinga kwa kushirikiana na wadau wengine kama Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori litaendelea na tafiti mbalimbali ili kuwezesha kutokomezwa kwa tatizo la tembo kuvamia makazi ya watu.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Vikosi Chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja, Jenerali Idd Nkambi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliwezesha Jeshi kupitia Mashirika yake kwa rasilimali fedha, vifaa na wataalam hivyo kulifanya JWTZ kutekeleza majukumu yake kwa weledi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.