Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mhe. John Elias Kwandikwa (Mb) amefanya ziara Makao Makuu ya muda ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyoko Msalato jijini Dodoma na kuzungumza na wakuu wa Matawi wakiongozwa na Mnadhimu Mkuu tarehe 08 Machi 2021.
Mhe. Waziri aliyapongeza Makao Makuu ya JWTZ kwa kuwajibika ipasavyo katika kuendesha Kisayansi Taasisi ya Ulinzi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu. Alipongeza pia ubunifu unaofanyika katika ngazi zote katika kutatua changamoto zilizopo.
Aidha, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ amemshukuru Mhe. Waziri Kwandikwa kwa kutenga muda wake na kutembelea Makao Makuu ya JWTZ pamoja na Kamandi zake na kujionea jinsi Jeshi linavyotekeleza Majukumu yake.
Pia, Waziri alipata fursa ya kutembelea eneo itakapojengwa Hospitali ya Jeshi Daraja la Nne kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kupewa taarifa ya hatua zilizochukuliwa na JWTZ kufanikisha kuanza kwa ujenzi huo muhimu ikiwa ni pamoja na kufikisha umeme na maji katika eneo la ujenzi.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.