Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi (Mbunge) leo tarehe 16 Novemba amefunga rasmi zoezi la Kijeshi la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki liitwalo Ushirikiano Imara 2018, Mlingano jijini Tanga.
Waziri alitoa pongezi kwa washiriki wote kwa kufanikisha malengo ya zoezi hilo yakiwemo Operesheni za Ulinzi wa Amani, Kupambana na Ugaidi, Kupambana na Uharamia, pamoja na Kukabiliana na Majanga.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo alisema Mazoezi hayo huongeza uimara wa Majeshi yetu katika kukabiliana na Matukio mbalimbali pindi wanapohitajika.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 9203 Dar es Salaam,
Street :Magore, Upanga
Fax : +255 22 2153432
Tel : +255 22 2150592- 4
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.