Zoezi lililoandaliwa kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki limefungwa rasmi tarehe 10 June, 2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Uganda na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kufungwa kwa zoezi hili kunafuatia kukamilika kwa mazoezi yaliyopangwa kufanywa kwa pamoja ya namna ya kushiriki Misheni na Oparesheni mbalimbali, kupambana na Ugaidi, Uharamia na Majanga mengine .
Aidha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax alihudhuria ufungaji wa zoezi hilo na kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa salamu za pongezi kwa mwenyeji Uganda kufanya maandalizi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushiriki zoezi hilo.
Nae Mkuu wa Utumishi Jeshini Meja Jenerali Paulo Kisesa Simuli kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi alipokea zawadi ya Ushiriki wa Kikundi cha Vyombo vya Ulinzi na Usalama cha Tanzania mara baada ya kufungwa zoezi hilo.
Ikumbukwe kuwa mazoezi haya yalifunguliwa rasmi 03 June, 2022 na washiriki wakiwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda ikiwa ni mwenyeji, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya, na Sudani Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa kama mtazamaji.
Tanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.