Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Utendaji Kivita Jeshini Brigedia Jenerali Alfred Kapinga ameongea na vyombo vya habari leo kuhusu zoezi la Ushirikiano Imara (CP EXERCISE) linalohusisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda.
Soma zaidiMajenerali 18 wa JWTZ waliostaafu kwa tarehe tofauti mwaka huu, waagwa rasmi leo katika sherehe iliyofanyika kwenye Kambi ya Twalipo Mgulani jijini Dar es Salaam.
Soma zaidiUjumbe kutoka Jeshi la Jamhuri ya Watu wa China ukiongozwa na Naibu Mnadhimu Mkuu Real Admiral Guan Bailin uliowasili na meli maalum ya matibabu nchini Novemba 19, 2017 leo Novemba 22 umemtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na kufanya mazungumzo ofisini kwake.
Soma zaidiMeli maalum ya kijeshi ya Jamhuri ya Watu wa China imewasili nchini jana Novemba 19, 2017 kwa ziara ya siku saba ikiwa na lengo la kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wa Tanzania.
Soma zaidiMkuu wa Majeshi ya Ulinzi Burundi Luteni Jenerali Niyongabo Prime leo Novemba 08, 2017 amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini Dar es Salaam, ziara hiyo imelenga kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya Majeshi ya nchi hizi mbili.
Soma zaidiMkuu wa Majeshi huyo alipokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo na kisha kufanya mazungumzo ofisini kwake
Soma zaidiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeaga miili ya marehemu Koplo Marcelino Pascal Fubusa na Praiveti Venance Moses Chiboni, leo tarehe 16 Octoba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.
Soma zaidiJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza vifo vya Askari wake wawili Koplo Maselino Paschal Fabusi na Praiveti Venance Moses Chiboni, ambao walikuwa katika Ulinzi wa Amani nchini DRC.
Soma zaidiTanzania People's Defence Forces,
P.O.Box 194 Dodoma,
Street : Miyuji, Msalato
Fax : +255 26 2962123
Tel : +255 737 962 064
E-mail : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Haki zote zimehifadhiwa. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.